Jumatatu, 16 Mei 2022

ZOGOLO MAKUNGANYA NO.8 ZOGOLO, MATAMBO, MBONDO NI NDUGU MOJA KOO MBALIMBALI.

 


ZOGOLO, MATAMBO, MBONDO NI NDUGU MOJA KOO MBALIMBALI.

Mlaluhombo alikuwa na mdogo wake waliozaliwa kwa mama mkubwa na mdogo, huyu mdogo aliolewa na bwana mmoja mwenye asili ya kijiji cha Disunyala kijiji kilichopakana na mji wa Mlandizi mkoa wa pwani nchini Tanganyika,  jina la mzee huyo lilitambulika kuwa ni Kondo lwinde, Kondo lwinde alizaa na mama huyo watoto wafuatao:-  Ally Kondo, Salumu Kondo na binti kondo watatu, lakini binti kondo hawa watatu; mkubwa wao alipata bahati ya kuolewa na mzee mmoja aitwae Shomvi Pazi na kuzaa nae mtoto aitwae Hazimala binti Shomvi, na baada ya hapo binti Kondo huyo aliachwa na kuolewa na mwanamme mwingine aitwaye Mohammedi Mbondo, hapa ndipo walipozaliwa Selemani mbondo, na mwingine aitwaye binti Mohamedi (King’amba),

Kwa msingi huu Hazimala binti Shomvi, na Selemani mbondo pamoja na binti Mohamedi (King’amba) hawa wote ni ndugu moja kutoka katika tumbo la binti Kondo mkubwa; lakini wakiwa baba zao ni mbalimbali.

Kati ya ndugu hawa; huyu aliyeitwa Hazimala binti Shomvi; alipata bahati ya kuolewa na mzee aitwae Kondo Matambo, ambapo alizaa nae watoto sita. wakwanza ni bi Mwajuma binti Kondo, wa pili ni Jumane Kondo, wa tatu ni Amini Kondo, wanne ni Stumai Kondo (mama Sele),   wa tano ni Asha Kondo (mama bovu), wa sita ni Pili Kondo. Asili ya Kizazi hiki unapokichunguza utaona kinatokea katika tumbo la mdogo wake Mlaluhombo; ambapo huyu Mlaluhombo ndiye  mama mzazi wa Mintanga Sefu, Selemani Sefu, Hadija Sefu, Athumani Sefu, Ally Sefu, na Chambuso Sefu. Watoto hawa walipatikana baada ya Mlaluhombo kuolewa na Sefu Zogolo.

Jumatatu, 12 Oktoba 2020

HALIMA SEFU CHAMBUSO


 

Picha hii ya Halima Sefu Chambuso inaonyesha umri wa miezi mitatu tangu kuzaliwa. 

 

Halima Sefu Chambuso alizaliwa tarehe 10/9/1996 katika mkoa wa pwani Tumbi Kibaha majira ya saa mbili asubuhi, Baba yake Halima anaitwa Sefu Chambuso Sefu Zogolo aliyezaliwa tarehe 4/10/1957 katika hospitali ya Sewa Hajji wilayani Bagamoyo mkoa wa pwani, na Mama yake Halima anaitwa Ziada binti Juma Mgeni Kondo aliyezaliwa tarehe 6/9/1977 katika Hospitali ya Tumbi kibaha pwani, Bi Ziada Juma baada ya kupata mimba; ilipofika siku ya tarehe 10 mwezi ule wa 9 mwaka 1996 asubuhi majira ya saa mbili na nusu; alihisi uchungu wa kujifungua; alichukuliwa haraka kupelekwa hospitalini Tumbi, walipofika usawa wa msitu mkubwa uliokuwepo wakati huo kama umbali wa mita miambili hadi kufika hospitalini hapo;  Ziada alizidiwa na uchungu wa kujifungua, mtu mmoja aliyekuwa akipita na baiskeli yake katika njia hiyo kwenda safari zake; baada ya kuyaona hayo alitoa msaada wa kwenda haraka hospitalini huko na kutoa taarifa kisha akamleta Dokta katika msitu huo na hatimaye Ziada binti Juma  kujifungua mtoto aliyeitwa Halima Sefu. Tangu siku hiyo baba yake Halima Mzee S. Chambuso aliutambua msitu huo kwa jina la msitu wa Halima, Ziada binti Juma alijifungua katika msitu huo wakiwa na Bi Asha binti Salehe ambae ni mama mzazi wa Ziada binti Juma ambae ndiye aliyemchukua kutoka nyumbani kwa dhamira ya kumuwahisha Hospitalini huko baada ya Ziada kuanza kuhisi uchungu wa kujifungua. 

Halima alilelewa jijini Dar es salaam wilaya ya Kinondoni kijiji cha Mwananyamala Kisiwani, baada ya kufika umri wa miaka minane  mwaka 2004 alianza shule ya msingi Mwananyamala Kisiwani na mwaka 2010 alimaliza shule ya msingi, mwaka 2011, alipata bahati ya kuendelea na masomo alipangiwa kuendelea na masomo katika shule ya sekondari ya Mabwe  alisoma hadi fom tu, na baada ya hapo alishindwa kuendelea kutokana na umbali wa shule ilipo, mwaka 2013 ilifanywa mipango ya kuendelea na masomo katika chuo cha kiislamu Ubungo Islamic akaendelea na masomo hatimaye alipata cheti cha Ualimu baada ya kufauru chuoni hapo, kwa msingi huo aliweza kupata nafasi ya kufundisha shule ndogo ya kwanza ya kiislamu iitwayo qaf iliyopo Mwananyamala B. jijini Dar es salaam.

   

 


 
 Halima S.Chambuso akiwa na cheti chake cha kufuzu ualimu
 
 
 
 
 
Picha hii inaonesha kitambulisho cha shule ya sekondari ya Mabwe pande aliposomea 
 
 

Halima S. Chambuso ni mtoto wa pili katika watoto waliozaliwa kwa mzee S.Chambuso na Bi Ziada binti Juma,  kabila halisi la Halima ni Mzalamo kwa baba yake na mama yake; unaweza kumjua vizuri Halima S. Chambuso  utakapofungua GOOGLE na kuandika maneno yafuatayo:- {ZOGOLO MAKUNGANYA NO. 5} unapofungua maneno haya utakuta kurasa iliyoandikwa :-        {Zogolo makunganya no 5 Sefu Zogolo} baada ya kuona maneno hayo utafuatilia fungu la 5.M, 

Na unaweza kufuatilia ukoo huo tangu ulipotokea kwa kuanza na Zogolo Makunganya no 1.

 

 

Halima S. Chambuso akiwa na dada yake Shakira S.Chambuso wakijionyesha kwenye picha.

 


Halima S.Chambuso akiwa na mama yake mzazi Bi Ziada binti Juma 

 


Halima S.Chambuso akimlisha keki mama yake 

 


Huyu ni baba yake Halima, mzee S. Chambuso Zogolo akijionyesha kwenye picha baada ya mazoezi.

KARIBU PWANI YETU

ZOGOLO MAKUNGANYA NO.8 ZOGOLO, MATAMBO, MBONDO NI NDUGU MOJA KOO MBALIMBALI.

  ZOGOLO, MATAMBO, MBONDO NI NDUGU MOJA KOO MBALIMBALI. Mlaluhombo alikuwa na mdogo wake waliozaliwa kwa mama mkubwa na mdogo, huyu mdogo al...