Ukoo wa zogolo
________________________________________
________________________________________
________________________________________

Katika safu za milima ya ulugulu watawala wa kilugulu walimkaribisha mgeni kutoka katika kabila la wazigua aliyekuwa akiitwa Kisabengo, Kisabengo alijishughulisha na uwindaji kwenye milima ya ulugulu, walugulu wakakubaliana na Kisabengo kuwa awe kinga yao kwa kuwahakikishia usalama wa walugulu wanaoishi huko; yaani Kisabengo aweze kudhibiti njia ya kasikazini inayotoka pwani kwenda bara kwa ajili ya kukinga maadui.

Ukoo huo wa Kisabengo ndiyo ulioasisi mji wa kwanza wa Mologolo uliopembezoni kidogo ya mlima, hapo mwanzo mji huo uliitwa mji wa Simbamwene.Kipindi kifupi baada ya mji kusikika; watu watano wageni walikuja kutoka masafa ya mbali; walipitia upande wa kulia ya mlima na kupiga kambi karibu na mji wa Simbamwene; baadae watu hawa walitambulika kuwa wawili ni watoto wa Zongobilo na wawili ni marafiki wa Zongobilo; watu hao walipokewa na utawala wa walugulu, inasadikika kuwa walitokea sehemu za Iringa na kupita miji kadhaa hadi kutokea Mologolo.
Historia inaonyesha kuwa binti wa chifu Kisabengo ndiye aliyekuwa akisimamia utawala wa mji huo, alishirikiana na wenyeji wote wa kilugulu akiwemo Zongobilo ambaye alipata hifadhi ya kuishi kama alivyokuwa akiishi Kisabengo na ukoo wake. Zongobilo alipoishi katika mji huo aliweza kujipatia mke aitwaye Mlasagala dada wa Chifu Ng'ohole aliyekuwa mganga mahili wa Mizimuni.
Zongobilo alizaa nae watoto wawili mmojawapo alimwita Makunganya.
Yatupasa tufahamu kwamba hii ni sehemu fupi ya historia iliyomtazama Zongobilo na familia yake kuingia Mologolo, kwakua mji huo wa Simbamwene wakati huo ulijengwa katikati ya mito miwili mikubwa yaani mto Mologolo na mto Ngelengele; mito hii ilileta mafuriko makubwa yaliyoufunika mji huo na kupoteza maisha ya sehemu kubwa ya watu akiwemo Zongobilo na mwanawe mmoja na rafiki zake wawili, ikumbukwe kuwa matukio haya yalitokea takribani miaka 21 kabla ya kuingia utawala wa kikoloni katika ukanda huo, kipindi cha baada ya mafuriko miaka ya 1880 wakazi waliobakia iliwapasa kuhamia pembezoni mwa mlima na wengine kuhamia sehemu ambayo hivi sasa inaitwa kinguluwila, na mtoto Makunganya pamoja na mama yake aitwaye Mlasagala walinusurika na kuelekea katika kijiji ambacho hivi sasa kinajulikana kwa jina la Msowelo, katika kijiji hiki Makunganya aliweza kuzaa watoto wafuatao:- mmoja aliitwa Dikuvale mwingine aliitwa Kingalu mwingine aliitwa Msunguli.
Makunganya hakuishia hapo aliterekia Ifakala katika kijiji cha Kisaki, akiwa Kisaki Makunganya alijitwalia mke na kujizalia watoto wawili mmoja aliitwa Adihungwa na wa pili alimrithisha jina la baba yake mkubwa yaani mtoto wa kwanza wa Zongobilo aliyemzaa akiwa Iringa sehemu za magharibi mwa milima ya welu aitwaye Zogolo.
Tafuta Zogolo Makunganya No.2 ukoo wa zogolo.
Nakala hii ni ya 1950. inalindwa na kuhifadhiwa na ukoo wa Zogolo.
_______________________________________
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni