Picha hii ya Halima Sefu Chambuso inaonyesha umri wa miezi mitatu tangu kuzaliwa.
Halima Sefu Chambuso alizaliwa tarehe 10/9/1996 katika mkoa wa pwani Tumbi Kibaha majira ya saa mbili asubuhi, Baba yake Halima anaitwa Sefu Chambuso Sefu Zogolo aliyezaliwa tarehe 4/10/1957 katika hospitali ya Sewa Hajji wilayani Bagamoyo mkoa wa pwani, na Mama yake Halima anaitwa Ziada binti Juma Mgeni Kondo aliyezaliwa tarehe 6/9/1977 katika Hospitali ya Tumbi kibaha pwani, Bi Ziada Juma baada ya kupata mimba; ilipofika siku ya tarehe 10 mwezi ule wa 9 mwaka 1996 asubuhi majira ya saa mbili na nusu; alihisi uchungu wa kujifungua; alichukuliwa haraka kupelekwa hospitalini Tumbi, walipofika usawa wa msitu mkubwa uliokuwepo wakati huo kama umbali wa mita miambili hadi kufika hospitalini hapo; Ziada alizidiwa na uchungu wa kujifungua, mtu mmoja aliyekuwa akipita na baiskeli yake katika njia hiyo kwenda safari zake; baada ya kuyaona hayo alitoa msaada wa kwenda haraka hospitalini huko na kutoa taarifa kisha akamleta Dokta katika msitu huo na hatimaye Ziada binti Juma kujifungua mtoto aliyeitwa Halima Sefu. Tangu siku hiyo baba yake Halima Mzee S. Chambuso aliutambua msitu huo kwa jina la msitu wa Halima, Ziada binti Juma alijifungua katika msitu huo wakiwa na Bi Asha binti Salehe ambae ni mama mzazi wa Ziada binti Juma ambae ndiye aliyemchukua kutoka nyumbani kwa dhamira ya kumuwahisha Hospitalini huko baada ya Ziada kuanza kuhisi uchungu wa kujifungua.Halima alilelewa jijini Dar es salaam wilaya ya Kinondoni kijiji cha Mwananyamala Kisiwani, baada ya kufika umri wa miaka minane mwaka 2004 alianza shule ya msingi Mwananyamala Kisiwani na mwaka 2010 alimaliza shule ya msingi, mwaka 2011, alipata bahati ya kuendelea na masomo alipangiwa kuendelea na masomo katika shule ya sekondari ya Mabwe alisoma hadi fom tu, na baada ya hapo alishindwa kuendelea kutokana na umbali wa shule ilipo, mwaka 2013 ilifanywa mipango ya kuendelea na masomo katika chuo cha kiislamu Ubungo Islamic akaendelea na masomo hatimaye alipata cheti cha Ualimu baada ya kufauru chuoni hapo, kwa msingi huo aliweza kupata nafasi ya kufundisha shule ndogo ya kwanza ya kiislamu iitwayo qaf iliyopo Mwananyamala B. jijini Dar es salaam.
Halima S. Chambuso ni mtoto wa pili katika watoto waliozaliwa kwa mzee S.Chambuso na Bi Ziada binti Juma, kabila halisi la Halima ni Mzalamo kwa baba yake na mama yake; unaweza kumjua vizuri Halima S. Chambuso utakapofungua GOOGLE na kuandika maneno yafuatayo:- {ZOGOLO MAKUNGANYA NO. 5} unapofungua maneno haya utakuta kurasa iliyoandikwa :- {Zogolo makunganya no 5 Sefu Zogolo} baada ya kuona maneno hayo utafuatilia fungu la 5.M,
Na unaweza kufuatilia ukoo huo tangu ulipotokea kwa kuanza na Zogolo Makunganya no 1.
Halima S. Chambuso akiwa na dada yake Shakira S.Chambuso wakijionyesha kwenye picha.
Halima S.Chambuso akiwa na mama yake mzazi Bi Ziada binti Juma
Halima S.Chambuso akimlisha keki mama yake
Huyu ni baba yake Halima, mzee S. Chambuso Zogolo akijionyesha kwenye picha baada ya mazoezi.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni