ZOGOLO, MATAMBO, MBONDO NI NDUGU MOJA KOO MBALIMBALI.
Mlaluhombo
alikuwa na mdogo wake waliozaliwa kwa mama mkubwa na mdogo, huyu mdogo aliolewa
na bwana mmoja mwenye asili ya kijiji cha Disunyala kijiji kilichopakana na mji
wa Mlandizi mkoa wa pwani nchini Tanganyika,
jina la mzee huyo lilitambulika kuwa ni Kondo lwinde, Kondo lwinde alizaa
na mama huyo watoto wafuatao:- Ally
Kondo, Salumu Kondo na binti kondo watatu, lakini binti kondo hawa watatu;
mkubwa wao alipata bahati ya kuolewa na mzee mmoja aitwae Shomvi Pazi na kuzaa
nae mtoto aitwae Hazimala binti Shomvi, na baada ya hapo binti Kondo huyo aliachwa
na kuolewa na mwanamme mwingine aitwaye Mohammedi Mbondo, hapa ndipo
walipozaliwa Selemani mbondo, na mwingine aitwaye binti Mohamedi (King’amba),
Kwa
msingi huu Hazimala binti Shomvi, na Selemani mbondo pamoja na binti Mohamedi
(King’amba) hawa wote ni ndugu moja kutoka katika tumbo la binti Kondo mkubwa; lakini
wakiwa baba zao ni mbalimbali.
Kati
ya ndugu hawa; huyu aliyeitwa Hazimala binti Shomvi; alipata bahati ya kuolewa
na mzee aitwae Kondo Matambo, ambapo alizaa nae watoto sita. wakwanza ni bi
Mwajuma binti Kondo, wa pili ni Jumane Kondo, wa tatu ni Amini Kondo, wanne ni Stumai
Kondo (mama Sele), wa tano ni Asha
Kondo (mama bovu), wa sita ni Pili Kondo. Asili ya Kizazi hiki unapokichunguza
utaona kinatokea katika tumbo la mdogo wake Mlaluhombo; ambapo huyu Mlaluhombo
ndiye mama mzazi wa Mintanga Sefu,
Selemani Sefu, Hadija Sefu, Athumani Sefu, Ally Sefu, na Chambuso Sefu. Watoto
hawa walipatikana baada ya Mlaluhombo kuolewa na Sefu Zogolo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni