ZOGOLO
MAKUNGANYA NO.1
1.A Katika
safu za milima ya ulugulu watawala wa kilugulu walimkaribisha mgeni kutoka
katika kabila la wazigua aliyekuwa akiitwa Kisabengo, Kisabengo
alijishughulisha na uwindaji kwenye milima ya ulugulu, walugulu wakakubaliana
na Kisabengo kuwa awe kinga yao kwa kuwahakikishia usalama wa waruguru
wanaoishi huko; yaani Kisabengo aweze kudhibiti njia ya kasikazini inayotoka
pwani kwenda bara kwa ajili ya kukinga maadui.
Ukoo
huo wa Kisabengo ndiyo ulioasisi mji wa kwanza wa Mologolo uliopembezoni kidogo
ya mlima, hapo mwanzo mji huo uliitwa mji wa Simbamwene.Kipindi kifupi baada ya
mji kusikika; watu watano wageni walikuja kutoka masafa ya mbali; walipitia
upande wa kulia ya mlima na kupiga kambi karibu na mji wa Simbamwene; baadae
watu hawa walitambulika kuwa wawili ni watoto wa Zongobilo na wawili ni
marafiki wa Zongobilo; watu hao walipokewa na utawala wa walugulu, inasadikika
kuwa walitokea sehemu za Iringa na kupita miji kadhaa hadi kutokea Mologolo.
Historia
inaonyesha kuwa binti wa chifu Kisabengo ndiye aliyekuwa akisimamia utawala wa
mji huo, alishirikiana na wenyeji wote wa kilugulu akiwemo Zongobilo ambaye
alipata hifadhi ya kuishi kama alivyokuwa akiishi Kisabengo na ukoo wake.
Zongobilo
alipoishi katika mji huo aliweza kujipatia mke aitwaye Mlasagala dada wa Chifu
Ng'ohole aliyekuwa mganga mahili wa Mizimuni.
Zongobilo
alizaa nae watoto wawili mmojawapo alimwita Makunganya.
Yatupasa
tufahamu kwamba hii ni sehemu fupi ya historia iliyomtazama Zongobilo na
familia yake kuingia Mologolo, kwakua mji huo wa Simbamwene wakati huo
ulijengwa katikati ya mito miwili mikubwa yaani mto Mologolo na mto Ngelengele;
mito hii ilileta mafuriko makubwa yaliyoufunika mji huo na kupoteza maisha ya sehemu
kubwa ya watu akiwemo Zongobilo na mwanawe mmoja na rafiki zake wawili,
ikumbukwe kuwa matukio haya yalitokea takribani miaka 21 kabla ya kuingia
utawala wa kikoloni katika ukanda huo, kipindi cha baada ya mafuriko miaka ya
1880 wakazi waliobakia iliwapasa kuhamia pembezoni mwa mlima na wengine kuhamia
sehemu ambayo hivi sasa inaitwa kinguluwila, na mtoto Makunganya pamoja na mama
yake aitwaye Mlasagala walinusurika na kuelekea katika kijiji ambacho hivi sasa
kinajulikana kwa jina la Msowelo, katika kijiji hiki Makunganya aliweza kuzaa
watoto wafuatao:- mmoja aliitwa Dikuvale mwingine aliitwa Kingalu mwingine
aliitwa Msunguli.
Makunganya
hakuishia hapo aliterekia Ifakala katika kijiji cha Kisaki, akiwa Kisaki
Makunganya alijitwalia mke na kujizalia watoto wawili mmoja aliitwa Adihungwa
na wa pili alimrithisha jina la baba yake mkubwa yaani mtoto wa kwanza wa
Zongobilo aliyemzaa akiwa Iringa sehemu za magharibi mwa milima ya welu aitwaye
Zogolo.
Tafuta
Zogolo Makunganya No.2 ukoo wa zogolo.
Nakala nyingine ya 1950.
