iliyoko sehemu ambayo hivi sasa inaitwa Iringa. Historia inaonyesha kuwa sehemu hiyo ya milima ya Welu ni maarufu kwa kabila la Wahafiwa; na upande wa magharibi ya milima hiyo wakati huo waliishi Walugulu; ambako ndiko atokako Zongobilo, na ndiko itokako asili ya Walugulu, hapa pana historia ndefu ya Walugulu kuwa na mji wa Mologolo.
Makuzi ya Zogolo wa kwanza yaliingia kwenye uindaji; safari za uindaji zilimpeleka milima ya ulugulu na kuteremkia kanda za pwani kulikomkutia vita vya mwaka 1850 kati ya Wazigua na Wakutu wakiongozwa na mtawala wa Pazi Mzongela kuwapiga Wakamba kutoka Kenya, Pazi Mzongela ambaye asili yake ni Ukutu ndiye wakati ule aliyekuwa ni mtawala wa Pwani ambaye makazi yake yalikuwa sehemu za Lukelele katika bonde la mto Ruvu Bagamoyo.
KwakuwaWakutu ni asili ya Ulugulu; Zogolo wa kwanza alijikita kwa ndugu zake Wakutu kuonyesha ushujaa wa kivita katika mapambano na Wakamba, na baada ya vita kwisha Pazi Mzongela alimpa uliwali pembezoni mwa Lukelele; maisha yake yaliishia huko na kuacha kizazi chenye asili ya Zogolo katika ukanda wa pwani mpaka leo.
nakala ya mwaka 1927.
