Alikuwa ni mtu mwenye nguvu
nyigi, Rangi ya ngozi yake ilikuwa ni
ya maji ya kunde.
Baada ya kuzaliwa Kisaki; makuzi
na maisha yake yalimpeleka katika kijiji cha Madimla, hicho ni kipindi cha
karne ya 19 takriban miaka ya 1900.
Alipokuwa Madimla aliweza
kupata kizazi; yaani familia, lakini hata hivyo baada ya utawala wa kikoloni Zogolo
aliitelekeza familia yake kutokana na hisia za kuwa utawala wa kikoloni uliotawala
kanda hiyo wakati huo hautaacha kumsumbua,
alitoroka na kwenda kujichimbia
katika kijiji cha Mngeta; huko alianza makazi mapya ambapo alijichukulia mke na
kuzaa watoto wakiwemo Mwinyimkuu Zogolo na Sefu Zogolo. Rehema Zogolo, Nuru Zogolo-{Tozi} Zakia zogolo, Kisamvu Zogolo.
Mwisho wa maisha yake
yalikuwa hapo hapo Mngeta Visima Saba. Akiwa ameacha watoto akiwemo Sefu
Zogolo.
nakala ya mwaka 1927.imehifadhiwa na kulindwa na wazee wa kale wa ukoo huu.
