Jumapili, 24 Machi 2019

ZOGOLO MAKUNGANYA NO.2 UKOO WA ZOGOLO

                     Ukoo wa Zogolo
________________________________________
________________________________________
________________________________________




2.A Zogolo Makunganya alikuwa ni mtu mwenye asili ya maumbile ya watu wa zamani, umbo lake lilikuwa kubwa; ni mwenye urefu wa Ft 6.30. Upana wa kutoka bega la kulia kwenda bega la kushoto ni Sm 20. alikuwa na muonekano wa kifua kipana; yaani ni pandikizi la jitu.
Alikuwa ni mtu mwenye nguvu nyingi, rangi ya ngozi yake ilikuwa ni maji ya kunde, Zogolo baada ya kuzaliwa Kisaki; makuzi na maisha yake yalimpeleka katika kijiji cha Madimla, haya yalikuwa ndani ya kipindi cha karne ya 19 takriban miaka ya 1900.  
Alipokuwa huko aliweza kupata kizazi yaani familia, lakini hata hivyo utawala wa kikoloni ulimsababisha Zogolo kuitelekeza familia yake kutokana na hisia za kuwa utawala wa kikoloni uliotawala kanda hiyo wakati huo hautaacha kumkamata kiutumwa, hivyo alitoroka na kwenda kujichimbia katika kijiji cha Mngeta; huko alianza makazi mapya ambapo alijichukulia mke na kuzaa watoto wa kiume wafuatao:-                        Mwinyimkuu Zogolo; Sefu Zogolo, na watoto wakike ni 1.Rehema binti Zogolo-Mwanamkulu; 2.Nuru binti Zogolo-Magati;                                  3.{Tozi}Zakia binti Zogolo-Kibule;              4.Kisamvu binti Zogolo-Kizuanda,              Mwisho wa maisha ya Zogolo yalikuwa hapohapo Mngeta Visima saba.          

Tafuta Zogolo Makunganya No.3 Sefu Zogolo.
                   imenakiliwa 1969.
_______________________________________

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KARIBU PWANI YETU

ZOGOLO MAKUNGANYA NO.8 ZOGOLO, MATAMBO, MBONDO NI NDUGU MOJA KOO MBALIMBALI.

  ZOGOLO, MATAMBO, MBONDO NI NDUGU MOJA KOO MBALIMBALI. Mlaluhombo alikuwa na mdogo wake waliozaliwa kwa mama mkubwa na mdogo, huyu mdogo al...